NAFASI ZA KAZI SERIKALINI

AFISA TARAFA – (NAFASI 145)


Nafasi hizi ni kwa ajili ya Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa katika
mikoa kama ifuatavyo:
Arusha (nafasi 4) , Dodoma (nafasi 11), Dar es Salaam (nafasi 1), Iringa (nafasi 3),
Kagera (nafasi 3), Kigoma (nafasi 7), Kilimanjaro (nafasi 12), Lindi (nafasi 11),
Manyara (nafasi 7), Mara (nafasi 1), Mbeya (nafasi 8), Morogoro (nafasi 3), Mtwara
(nafasi 9), Mwanza (nafasi 5), Pwani (nafasi 6), Rukwa (nafasi 12), Ruvuma (nafasi
14), Shinyanga (nafasi 8), Singida (nafasi 4) Tabora (nafasi 6) na Tanga (nafasi 10).


MAJUKUMU YA KAZI

1. Kwenye Mamlaka ya Serikali Kuu.
- Kumwakilisha na kumsaidia Mkuu wa Wilaya katika utekelezaji wa shughuli za Serikali Kuu katika Tarafa.
- Kuandaa na kuratibu taarifa na ripoti zinazohusu masuala ya ulinzi na usalama ya kata kwenye tarafa yake na kuiwasilisha kwa Mkuu wa Wilaya.
- Kuhamasisha na kuhimiza wananchi iliwashiriki kwenye shughuli za maendeleo kwenye Tarafa.
- Kuwa kiungo kati ya Serikali kuu na Wananchi Katika Tarafa.
- Kuwa mlinzi wa amani katika eneo lake.
- Kufuatilia na kuhimiza utekelezaji wa sera za Serikali katika eneo lake na kuhakikisha kuwa zinatekelezwa ipasavyo.
- Kuratibu shughuli zote za maafa na dharura mbalimbali katika eneo lake
- Kuandaa taarifa zote zinazohusu masuala ya Serikali Kuu kuhusu utendaji wa kazi za maafisa Watendaji wa kata wa eneo lake na kuziwasilisha kwa Mkuu wa Wilaya.
- Kuwa kiungo kati ya Serikali kuu na Serikali za Mitaa. katika eneo lake.
- Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Katibu Tawala wa Wilaya.


2. Kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa;
- Kuwasaidia Wakurugenzi wa Serikali za Mitaa katika shughuli za Maendeleo katika eneo lake
- Kusimamia utendaji wa shughuli za Maafisa Watendaji wa Vijiji, Kata na Mitaa.
- Kushiriki na kutoa ushauri katika upangaji wa mipango ya Maendeleo katika eneo lake
- Kuhudhuria vikao vya kamati za Halmashauri na Baraza la madiwani na kutoa ushauri.
- Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake kama zitakavyopokelewa kutoka kwa Watendaji wa Kata.
- Kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogondogo za Halmashauri ya Wilaya, Miji, Manispaa au Jiji.


SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu katika mojawapo ya fani za Sheria,Menejimenti,Utawala,Sayansi ya Jamii, Kilimo, Mifugo,Ushirika, Mazingira, au Maji kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D kwa mwezi.

Maombi yatumwe kwa anuani ifuatayo:

Katibu
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
S. L. P 63100,
DAR ES SALAAM.

Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 14 Mei, 20120 comments:

Post a Comment

Please Click the Like Button Below To Join Our Facebook Page and receive all updates