SHIRIKISHO LA VYAMA VYA WAFANYAKAZI TANZANIA ( TUCTA) NAFASI ZA KAZI

Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) linatangaza nafasi za ajira kwa watanzania wenye sifa.

1. MKURUGENZI WA ELIMU

SIFA
- Mwenye Shahada ya Pili katika nyanja za Elimu, Mahusiano kazini, Ustawi wa Jamii, Rasilimali watu au Sosholojia
- Mwenye mafunzo ya Utoaji wa Elimu (Teaching methods)
- Mwenye umri usiozidi miaka 45
- Mwenye kufahamu vizuri lugha ya Kiswahili na Kiingereza, kuandika na kuzungumza
- Mwenye kufahamu vizuri matumizi ya Kompyuta
- Mwenye uzoefu wa miaka mitano (5) na kuendelea

2. AFISA MCHUMI NA MCHAMBUZI WA SERA (ECONOMIST AND POLICY ANALYST)

SIFA:
- Mwenye Shahada ya Pili au Diploma ya Uzamili katika nyanja za Uchumi, Utafiti, Mipango na Sera.
- Mwenye umri usiozidi miaka 45
- Mwenye uwezo mkubwa wa matumizi ya Kompyuta
- Mwenye uzoefu wa miaka mitano (5) na kuendelea

3. MSAIDIZI KUMBUKUMBU MWANDAMIZI (RECORDS MANAGEMENT ASSISTANT)

SIFA
- Diploma ya Kawaida katika fani ya Urasimu Ramani kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali
- Mwenye ujuzi wa Kompyuta na uzoefu wa kazi usiopungua miaka mitano (5)

Mishahara na marupurupu -ni ya kuvutia kwa kuzingatia Utendaji.

NAMNA YA KUTUMA MAOMBI
Barua za maombi zikiambatana na wasifu (CV) ziandikwe kwa:-

Katibu Mkuu
TUCTA,
S.L.P 15359,
Barua Pepe : tucta2012@yahoo.com

Mwisho wa kupokea Maombi ni tarehe 05 Oktoba, 2012.

0 comments:

Post a Comment

Please Click the Like Button Below To Join Our Facebook Page and receive all updates