TAASISI YA BENJAMIN WILLIAM MKAPA HIV/AIDS TANGAZO LA KAZI

Katika kuchangi jitihada za serikali za kuboresha utoaji na upatikanaji wa huduma bora za Afya, Taasisi ya Benjamin William Mkapa HIV?AIDS Foundation (BMAF) imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa "Mkapa Fellows" tokea mwaka 2005.

Katika kuendeleza jitihada hizi, Taasisi ya mkapa Foundation kwa kushirikiana na Abbott Fund Tanzania inatekeleza mradi wa kuimarisha huduma za Afya kwenye Maabara za Hospitali za Mikoa Ishirini na tatu (23). Moja ya Malengo ya mradi huu ni kuongeza wataalam wa maabara (Fellows) katika maabara za miko ambazo zimeboreshwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Abbott Fund Tanzania, na kuwa za kisiasa. Katika mwaka wa fedha 2011/2012, Mradi huu uliajiri Wateknolojia wa Maabara 60 waliopangiwa kazi katika Hospitali za Mikoa 10.

Katika awamu ya kwanza ya mwaka 2012/2013, mradi unalenga kuajiri Watunza Kumbukumbu Saba (7) watakaopangiw katika hospitali za Mikoa ya ; Lindi, Mtwara, Pwani, Kigoma, Tabora, Shinyanga na Kagera.

WATUNZA KUMBUKUMBU

SIFA KWA WAOMBAJI
- Stashahada au cheti cha utunzji wa kumbukumbu (Records management) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali
- Ujuzi na uzoefu wa kutumia programu mbalimbali za kompyuta
- Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 30 ifikapo tarehe ya mwisho wa tangazo hili

MAOMBI YAAMBATANISHWE NA;
1. Barua ya maombi ya kazi, ikipendekeza hospitali mwombaji anayopendelea kupangwa kazi na pia aonyeshe ridhaa ya kujiunga na Utumishi wa Umma, baada ya mkataba wa miezi 16 kumalizika
2. Nakala ya cheti cha Taaluma na chati cha Kidato cha 4 na 6 (iwapo anacho) na viwe vimethibitishwa na Hakimu au Wakili
3. Picha mbili (2) - saizi ya Pasipoti na maelezo binafsi (CV), ikionyesha umri, anuani kamili na namba ya simu ya kiganjani, pamoja na anuani/ namba ya kiganjani ya wadhamini wako.

Maombi yote yatumwe kwa;
Afisa Mtendaji Mkuu
Benjamin William Mkapa HIV/AIDS Foundation,
S.L.P 76274
Kiwanja Na. 372,
Barabara ya Chole,
Masaki -Dar es Salaam

Au kwa Barua Pepe : info@mkapahivfoundation.org

MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI HAYA NI TAREHE 15 JANUARI, 2013

Chanzo : DailyNews 20/12/2012

0 comments:

Post a Comment

Please Click the Like Button Below To Join Our Facebook Page and receive all updates